Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (UN) limekataa azimio lililoungwa mkono na Marekani la kuiwekea vikwazo vya silaha taifa la Sudan Kusini.

Azimio hilo lilipata kura saba ya kura 15 na kukosa kufikisha kura tisa ambazo zinahitajika kupitishwa azimio.

Nchi nane zikiwemo Urusi,China na Japan hazikupiga kura kutokana na sababu zao binafsi katika mchakato huo.

Mapigano kati ya vikosi watiifu kwa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na makamu wa rais aliyefutwa kazi Riek Machar, yalizuka mwezi Disemba mwaka 2013 na kusababisha nchi hiyo kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *