Kiungo wa klabu ya Chelsea, Tiemoue Bakayoko amepata ajali mbaya ya gari jana jioni katika eneo la Blundel Lane wakati akitoka mazoezini akirudi nyumbani.

Bakayoko (23) alipata ajali hiyo dakika 5 baada ya kutoka mazoezini akiwa na gari yake aina ya Mercedes Benz G63 AMG SUV baada ya kuyumba na kuacha njia.

Hata hivyo, kaka wa mchezaji huyo ajulikanaye kwa jina la Namory amesema Bakayoko hajaumia sana kwenye ajali hiyo.

Namory amesema kuwa walikuwa wote kwenye gari na alimuachia Bakayoko aendeshe lakini baadae akamuona akishindwa kuliongoza gari kwa kukosa uzoefu kutokana na sheria za Uingereza kuendesha upande wa kushoto wa barabara ndipo akaacha njia na kuingia mtaroni.

Bakayoko alijiunga na klabu ya Chelsea akitokea AS Monaco kwa dau la Euro milioni 40 na mpaka sasa amecheza mechi sita akiwa na Chelsea na kufunga goli moja.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *