Mwanamuziki na muigizaji wa Bongo Movie, Baby Madaha amewataka mastaa wenzake kurudi shule kutokana na ugumu wa maisha pamoja na dunia kuendelea.

Baby Madaha anayeunda Kundi la Scorpion Girls amesema kutokana na maisha kuwa magumu na kazi za sanaa hazilipi hasa filamu, mastaa hasa wa kike wanatakiwa kuachana na tabia za kujiuza kwa wanaume hovyo na kurudi darasani kwani elimu ndiyo itawakwamua kimaisha.

kweli

Madaha amesema kuwa “Wakati nasoma watu walikuwa wananicheka, sasa nakula mshahara kwenye kampuni ya madini ambayo tunamiliki mimi na kaka yangu yenye matawi hapa Dar na Dubai’.

Mkali huyo amesema kuwa ‘Sijiuzi China wala  Dubai kama wasanii wengine, yaani mastaa lazima mrudi shule maana ‘vyuma’ vimekaza vibaya,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *