Wasanii wamemwagia sifa meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale kutokana na mchango wake anaofanya katika muziki wa Bongo Fleva.

Msanii wa Bongo Fleva, Dreygon kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika ‘Ni ukweli usiopingika Babu Tale amefanya jitihada kubadilisha hii kazi iliyokuwa iitwa ya kihuni kuwa inatambulika sasa na wasanii wanaendesha Maisha yao kupitia tasnia hii”.

Ameongeza ‘Kuna hata baadhi ya vyuo duniani sasa wanatumia muziki huu kufundishia lugha ya Kiswahili. Hatuwezi kumtaja Diamond tukaacha kumtaja Babu Tale. Mnyonge mnyongeni haki zake mpeni’.

Kauli ya msanii huyo imekuja baada ya baadhi ya watu wanasema kuwa kuwa meneja huyo wa WCB hakuna kitu alichofanya katika muziki wa Bongo Fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *