Meneja wa mwanamuziki, Diamond Platnumz, Babu Tale amesema kuwa mwenye jukumu la kujua alipo Roma ni mkuu wa mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana yeye ndiyo mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

Kupitia akaunti yake ya Instagram meneja huyo amesema kuwa wamezunguka vituo vyote vya Polisi na mwanamuziki huyo hayupo.

Babu Tale ameongeza kuwa kuwa kutokana na hayo mwenye jukumu la kujua alipo Roma na wenzake ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Babu Tale ameandika kama ifuatavyo

Uoga ni uzembe me nazani mwenye jukumu la kujua Roma yupo wapi ni Mkuu wa Mkoa sababu yeye ndio kiongozi wa kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa sasa ikiwa tumezunguka vituo vyote vya polisi na mwenzetu atumuoni nani wa kumfuata kumwambia tunamtaka mwenzetu kama sio @paulmakonda me naanza hili bila uoga mkuu wa mkoa naomba utusaidie kutuambia mnzetu @roma2030 alipo.

Pia meneja huyo ameendelea kuandika Tukutane Tongwe mida hii me nipo kwa foleni wakuu #uogauzembe#freeroma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *