Meneja wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na kundi la Tip Top Connection, Hamis Tale Tale maarufu kama Babu Tale amefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Babu Tale amefikisha katika mahakama hiyo ili kutoa sababu za kwanini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya shilingi milioni 250 kwa makosa ya kuvunja sheria ya hakimiliki.

mondi

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Sheikh Mbonde kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya sheikh huyo jambo ambalo ni kinyume na hakimiliki.

Hapo awali mahakama ilimuamuru Babu Tale amlipe Sheikh Mbonde kiasi cha shilinigi milioni 250 kwa kosa la kuuza na kusambaza nakala za mawaidha bila idhini ya Sheikh huyo jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Kutokana na hukumu hiyo Babu Tale alikaidi kumlipa sheikh Mbone ivyo mahakama imeamuru akamatwe na afikishwe mahamani hapo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *