Nguza Viking maarufu kama ‘Babu Seya’ na mwanae Jonson Nguza ‘Papii Kocha’ ambao kwa sasa wanatumikia kifungo cha maisha gerezani wanatarajia kutoa burudani kesho kwenye tamasha la wafungwa litakalofanyika katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi.

Katika tamasha hilo Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ itakuwepo kutoa burudani sambamba na wanamuziki hao maarufu wanaotumikia kifungo cha maisha jela.

Pia mwanamuziki wa Singeli, Msaga Sumu atatoa burudani kwenye tamasha hilo la kuwatia moyo wafungwa.

Lengo la tamasha hilo ni kuwatia moyo wafungwa na kuwaonesha kwamba wapo pamoja na Watanzania wenzao ambao wanaishi huru.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen Mwaisabila naye anatarajiwa kutoa neno katika tamasha hilo sanjari na viongozi wengine wa magereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *