Baba mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Belle 9 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kugongwa na boda boda mkoani Morogoro.

Meneja wa mwanamuziki huyo Jahz Zamba amethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mzee Damian kwa kugingwa na boda boda.

Zamba amesema kuwa baada ya ajali hiyo mzee Damian alivunja mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa hospitali.

Pia amesema kuwa Dereva wa boda boda naye ameumia vibaya ikiwemo kuvunjika taya na kujeruhiwa kichwa.

Jahz amesema baada ya Mzee Damian kupelekwa hospitali na kuwekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahtuti, kuna dawa zilikuwa zikihitajika lakini zilikosekana kwenye hospitali hiyo.

Amesema kaka yake Belle anayeishi Morogoro aliingia mtaani kuzisaka na aliporudi mida ya saa sita usiku alikuta Mzee ameshafariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *