Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Haji Adam ‘Baba Haji’ amesema kuwa hakuwai kushiriki rushwa ya ngono licha ya vitendo hivyo kukthiri ndani ya tasnia ya filamu hapa nchini.

Baba Haji amesema kuwa mabinti wengi wenye ndoto za kuigiza, hutumia mbinu mbalimbali ili kupata nafasi za kuigiza kwenye movie za wasanii wakubwa na mbinu mojawapo ni kuwa tayari kutoa rushwa hiyo kwa wahusika ili kupata nafasi.

Muigizaji huyo alitolea mfano wake kwa muigizaji nyota wa Bongo movie, Aunt Ezekiel ambaye yeye ndiyo aliyemtambulisha kwenye ulimwengu wa filamu kupitia movie ya Miss Bongo iliyotoka miaka ya nyuma na kutamba lakini hakuomba rushwa ya ngono kwa Aunt Ezekiel.

Kwa upande mwingine Baba Haji ameonesha kupingana na wanaodai kuwa Bongo Movie inaporomoka huku yeye akipinga na kusisitiza kuwa kwa sasa tasnia ya filamu nchini inakua na wasanii wanapata mafanikio.

 

Pia alitumia nafasi hiyo kukanusha tetesi za kuoa mke mwingine akisema kuwa mke ni mmoja tu na ndiye aliyefunga naye ndoa, lakini waliachana baada ya mwaka mmoja wa ndoa na kwa sasa hawako pamoja tena, isipokuwa anahudumia mtoto waliozaa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *