Baada ya kuenea taarifa za mrembo, Hamisa Mobeto kuzaa na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, baba mzazi wa Diamond afunguka kwa kusema ni vema Diamond akamuoa Hamisa.

Kauli hiyo amesema jana wakati akifanyiwa mahojiano na kituo cha TV maarufu nchini kuhusu tetesi hizo za mwanawe kuzaaa na mwanamitindo huo.

Alipoulizwa kuhusu Zari, baba mzazi huyo amefunguka kwa kusema kuwa ni vema Daimond akawaoa wanawake wote yani Zari pamoja na Hamisa Mobeto kwasababu wamemzalia watoto.

Hamisa and Zari
Hamisa and Zari

Kuhusu mtoto wa Hamisa kupewa jina lake ambalo ni Abdul,Baba mzazi wa Diamond amesema kuwa kama Diamond ameamua kumpa mtoto huyo jina lake ni upendo na inaonesha thamani kwake.

Baba Diamond amesema hawezi kumlaumu Diamond kwa kilichotokea kwani yeye ni msanii mkubwa anakumbana na vishawishi mbalimbali.

Mpaka sasa Diamond hajawahi kutoa neno lolote juu ya mtoto huyo licha ya mama yake pamoja na dada yake Esma kuonekana mara kadhaa wakimtembelea mrembo aliyejifunga siku chache zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *