Baba mazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Athuman Omary ‘Harmorapa amefunguka na kudai kwamba mwanae huyo aligoma kujiunga na jeshi alipomaliza kidato cha nne kwa madai ya kutaka kufanya muziki licha ya kuwa tayari alikwisha tafutiwa nafasi.

Baba mzazi huy amesema kuwa alipoona mtoto wake amekataa nafasi hiyo ya jeshi hakutaka kumlazimisha bali ilibidi akubaliane naye kwani hakutaka kumkatisha kwenye kutimiza ndoto zake.

Baba mzazi huyo amesema kuwa “Athuman alisoma shule kuanzia la kwanza mpaka la saba, baada ya hapo alikwenda form one mpaka four ila alipomaliza nilimtafutia nafasi ya kujiunga jeshini lakini alinikatalia.

Pia amesema kuwa “Mimi kama mzazi sikutaka kumlazimisha nikasema ngoja nimuache labda ana ndoto zake. Ila nilimwambia kwenye muziki huko kunahitaji pesa na mimi pesa sina akaniambia baba usijali nitapambana na kweli nikamuacha” – baba yake Harmorapa alifunguka”.

Mbali na hilo mzazi huyo amesema suala la mwanaye kuonekana na kiki yeye anaona si kibaya sababu hakuna jambo baya ambalo amelifanya, na kusema anaamini muziki ndiyo unahitaji mambo hayo ila siku akiona kuna kitu kibaya amefanya atamwita na kumweleza.

Kwa upande wake Harmorapa amesema kuwa ipo siku atakuja kumfanyia jambo kubwa baba yake huyo mzazi ambaye anaishi jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *