Baadhi ya wanachama wa NCCR-Mageuzi wamemtaka Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia na Katibu Mkuu wa chama hicho, Martin Danda kujiuzulu ndani ya siku tatu kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwamo ubadhirifu wa fedha na kutaka kukiua chama hicho.

Mbatia anadaiwa kuuza mali za chama zikiwamo nyumba mbili zilizoko jijini Dar es Salaam eneo la Bunju B, moja iliyoko Tarime mkoani Mara na shamba la ekari 56 lililoko Bagamoyo mkoani Pwani.

Faustine Sungura mmoja wa wanachama wa chama hicho, amesema mbali na kuuza nyumba pia Mbatia ana mkakati maalumu wa kuiua NCCR na kuhamia Chadema ambako ameahidiwa ukatibu Mkuu.

Pamoja na mambo mengine Sungura amesema viongozi hao wasipojiuzulu atawafungulia mashtaka mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *