Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amesema kuwa yupo kwenye hatua za mwisho za mchakato wa kuingia mkataba na ‘record label’ ya Rockstar4000.

Nuh amesema kuwa haitakuwa busara kila kitu kikawekwa wazi kabla ya makubaliano ya kusaini lakini mashabiki wakae wakijua yupo njiani kujiunga na lebo hiyo.

Amesema kuwa “Ni kweli nipo kwenye mazungumzo na lebo ya Rockstar4000 ambayo yupo Kiba na soon nitasaini mkataba.

Pia amsema kuwa Nimekubali kufanya hivyo kwa sababu Kiba ni mtu wangu wa karibu na ninamheshimu kama kaka yangu, naamini tutafanya kazi vizuri tukiwa pamoja huko na hakuna nitakacho-pungukiwa kwa kuminywa kivyovyote vile,”.

Lebo hiyo pia ina wasanii wengine akiwemo Lady Jaydee, Ommy Dimpoz pamoja na Barakah The Prince pamoja na Alikiba ambaye amechaguliwa kuwa mkurugenzi wa muziki wa lebo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *