Muigizaji wa Bongo movie, Daudi Michael maaarufu kwa jina la Duma anatarajia kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Chun’tama hivi.

Duma amesema kuwa filamu hiyo itakuwa inazungumzia maisha halisi ya watanzania pamoja na masuala ya uchawi na mambo mengine mengi.

Muigizaji huyo amesema “Baada ya kufanya vizuri katika filamu yangu ya ‘Mchongo Sio’ nikaona nisikae kimya sana kwahiyo nimeamua kuachia filamu mpya inaitwa Chun’tama”.

 Mbali na Duma waigizaji wengine kwenye filamu hiyo ni Grace Mapunda, Chuchu Hans, Hashim Kambi, Suleiman Barafu na wengineo.

Vile vile Duma amesema kuwa hataki kuwaangusha mashabiki wake wa filamu ndiyo maana hataki kukaa muda mrefu bila kuachia filamu mpya.

Msanii huyo aliwahi kutamba kwenye tamthilia ya Siri Ya Mtungi iliyojizolea umaarufu baada ya kufanya vizuri katika soko la tamthilia nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *