Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane amesema timu hiyo imelamba dume kwa kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton.

Keane amesema hayo baada ya nyota huyo wa Ubeligji kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa 4-1 ilioupata Man United dhidi ya CSKA Moscow kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya jana usiku.

“Ni mchezaji mwenye kiwango cha juu sana ambaye kumnunua kwa £75 milioni ni biashara ya faida kwa United’.

Mkongwe huyo wa Man United ameongeza kuwa umri wa Lukaku pamoja na uwezo wake unaweza kukubali tu kuwa kumnunua kwa bei hiyo ni makubalino tu ya pande mbili lakini alistahili zaidi.

Lukaku amesajiliwa msimu huu akitokea Everton na tayari ameshafunga mabao 10 katika michezo 9 kwenye mashindano yote aliyoichezea Manchester United.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *