Mkali wa Bongo Fleva, Chege Chigunda kutoka TKM Wanaume Family amesema kuwa anajipanga kuachia albam mpya.

Chege amesema albam hiyo itauzwa kupitia mitandao ya kijamii pamoja na mtandao wa kuuza muziki wa Wasafi.com chini ya Diamond Platnumz.

Mwanamuziki huyo amedai anaamini albamu hiyo itafanya vizuri sokoni kutokana na vitu vikubwa alivyoviandaa kwenye albamu hiyo pamoja na kolabo za kimataifa.

Chege akiwa na Temba
Chege akiwa na Temba

Kuhusu project yake na Temba ‘Go Down’  Chege amesema kuwa imeenda vizuri sana kutokana na kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Kwa upande mwingine Chege amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuingojea albam hiyo baada ya kumaliza project za TMK akiwa na Temba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *