Kingozi wa kundi la Yamoto Band, Temba amesema kuwa kundi hilo linatarajia kuachia nyimbo mbili kwa pamoja baada ya kukamilika kwa nimbo hizo.

Temba ambaye ni mwanamuziki mkongwe amefunguka na kuweka wazi mipango ya kundi hilo na kusema wapo tayari kuachia kazi mbili ndani ya siku mbili zijazo.

Kiongozi huyo amesema alikuwa na mpango wa kuachia kazi yake lakini inabidi asubiri kwanza Yamoto Band watoe kazi zao kwani ni muda mrefu sasa hawajaachia kazi na wananchi wanawasubiri.

Temba amesema kuwa Yamoto Band wamekaa sana kimya kama miezi sita bila kutoa nyimbo mpya hivyo mahitaji ya mashabiki ni kuwasikia Yamoto Band.

Kundi hilo limekaa kimya bila kutoa nyimbo huku kitendo hiko kikihusishwa na kutoelewana kati ya mkurugenzi wao Said Fella (Mkubwa Fella) na vijana pamoja na meneja wao Chambuso.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *