Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye kundi kongwe la muziki wa Bongo Fleva, Unique Sisters limerudi tena rasmi kwenye muziki huyo.

Kundi hilo lenye wanamuziki watatu wa familia moja lilijizolea umaarufu mkubwa katika anga ya muziki wa Bongo Fleva miaka ya 2000 kutokana na uhodari katika uimbaji.

Mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo Rahima ambaye ndiye mkubwa amesema kuwa walikuwa kimya kutokana na majukumu ya kifamilia ambapo wawili kati yao wameshaolewa, lakini wameona kiu ya mashabiki imekuwa kubwa na kuanza wataachia kibao kitakachoitwa ‘Kwako Wewe’.

Rahima amesema kuwa wameamua kurudi tena kwenye game ya muziki wa Bongo Fleva kutokana na maoni ya mashabiki wao kuwataka kurudi kwenye muziki huo baada ya kukosa huduma ya wasanii hao kwa muda mrefu.

Kwa upande wa Radhina ambaye ndiye mdogo kwenye kundi hilo amesema pia wamekuja kuleta ladha tofauti ya muziki ili kuleta changamoto zaidi kwenye game upande wa wanawake kutokana na kukosa changamoto.

Pia wasanii hao wameendelea kwa kusema kwamba wamefurahi kuona jinsi game ilivyobadilika siku hizi na kuwa na wasanii wengi wa kike, tofauti na kipindi cha nyuma ambapo wasanii wa kike walikuwa wachache.

Kundi hilo la Unique Sisters linaundwa na ndugu wa familia moja, Rahima Kipozi, Radhia Kipozi na Radhina Kipozi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *