Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Joslin ametangaza kurudi tena kwenye muziki baada ya kuanza kufanya video ya wimbo wake mpya ‘Only you’ ambao anatarajia kuuachia hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Joslin aliandika juu ya ujio wake huo mpya baada ya kuandika “Yeah…the return of Joslin…(ndoto yao) “.

Pia video Queen ambaye anamefanya video hiyo Proyanca Michael alifunga na kusema kuwa anatambua watu wamemkumbuka sana hivyo ni wakati wake kurudi na ngoma hiyo mpya ‘Only You’.

Joslin aliwahi kutamba miaka ya nyuma kwenye anga ya muziki wa Bongo fleva kutokana na nyimbo zake kuwabamba mashabiki, miongoni mwa nyimbo hizo ni ‘Kifo’ pamoja na ‘Niite basi’ ambao ndiyo ulikuwa habari ya mjini wakati huo.

Vile vile Joslin alikuwa miongoni mwa waliounda kundi la Wakali Kwanza akiwa na wasanii wenzake kama Makamua na Qj.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *