Uongozi wa studio ya B Hits umesema kuwa hawana mpango wa kuwasajili wasanii wengine au kuwarudisha wanamuziki waliokuwa chini ya lebo hiyo yenye maskani yake Mbezi jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa studio hiyo Aman Joachim amesema kuwa wamejifunza kutokana na makosa kutokana na kuwekeza pesa nyingi kwa wasanii walikuwa chini ya lebo hiyo na kutoambulia chochote.

Pia Joachim amewataka wasanii kupuuza taarifa zinazosemwa kuwa studio hiyo inatoza pesa nyingi kitu ambacho siyo kweli na gharama zake kama kawaida.

Baadhi ya wasanii waliokuwa chini ya lebo hiyo ni Vanessa Mdee, Jux, M Rap Mabeste na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *