Klabu ya Azam FC imesitisha mikataba ya makocha wake kutoka nchini Hispania kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwasasa.

Uamuzi huo umefanywa na bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo pamoja na jopo la makocha hao wakiongozwa na kocha mkuu, Zeben Hernandez, kocha msaidizi, Yeray Romeo, kocha wa unapen Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na Mtaalamu wa tiba za Viungo, Sergio Perez.

Kocha huyo Hernandez ameingoza Azam Fc mechi 18 ambazo ni za mashindano, 17 za ligi na moja ya Ngao ya Jamii amefanikiwa kushinda mechi nane, sare sita na kufungwa mara nne.

Kikosi cha Azam FC kwasasa kitakuwa chini ya makocha wa timu ya vijana ya timu hiyo, Idd Cheche na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar.

Azam Fc leo watashuka dimbani dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Azam Complex, Chamanzi jijini Dar es Salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *