Baada ya kuwatimua makocha wake kutoka nchini Hispani hatimaye Azam FC imemtambulisha kocha mpya atakayeinoa klabu hiyo ambaye jina lake anaitwa, Aristica Cioaba kutoka nchini Romania.

Kutokana na makubaliano ya pande zote mbili kocha huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Zeben Hernandez.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd amesema Aristica Cioaba atasaidiwa na makocha wazalendo ambao wanaiongoza Azam kwa sasa wakiongozwa na Idd Cheche.

Makocha ambao waliopewa nafasi kuinoa klabu hiyo ni Karl Ongala ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo akiwa mchezaji na kocha msaidizi akarejeshwa kwenye benchi la ufundi la Azam FC miaka ya nyuma.

Kocha mwingine ni Mkwasa pia ni miongoni mwa makocha waliotajwa kupewa jukumu la kuinoa Azam baada ya kuachana na timu ya taifa ya Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *