Azam FC imemsaini kiungo mshambuliaji  kutoka klabu ya Medeama ya Ghana Enock Atta Agyei kwa mkataba wa miaka mitatu.

Azam FC iliingia makubaliano maalumu na Medeama ya Ghana juu ya kumsajili kinda huyo anayetimiza umri wa miaka 18 mwakani baada ya benchi la ufundi kuridhishwa na uwezo wake na sasa amejiunga rasmi kwenye viunga vya Azam Complex.

Agyei amesaini mkataba tayari kuanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) mwakani pamoja na michuano mingine ikiwemo Kombe la Shirikisho Afrika.

Pia Azam imewapokea wachezaji saba kwenye majaribio ya kujiunga na klabu hiyo, ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),

Wengine ni washambuliaji Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *