Kampuni ya Azam limeingia mkataba mpya na shirikisho la soka nchini (TFF) kwaajili ya kuendelea kurusha moja kwa moja mechi za ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara kwa miaka mitano.

Mkataba huo wenye thamani ya shilingi bilioni 23 utazinufaisha timu zinazoshiriki ligi kuu pekee.

Timu hizo zinatarajia kupata jumla ya shilingi milioni 126 kila moja kwa kila mwaka ambayo ni ongezeko la shilingi milioni 26 kutoka katika mkataba wa awali.

Timu zitakazoshiriki ligi kuu Tanzania bara msimu ujao ni:

African Lyon, Azam FC, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Majimaji FC, Mbao FC, Mbeya City, Mtibwa Sugar, Mwadui FC,  Ndanda FC, Ruvu Shooting, Simba, Stand United, Tanzania Prisons, Toto Africa na mabingwa watetezi Yanga

Tido Mhando: Mkurugenzi wa Azam Media akikabidhi mfano wa hundi kwa katibu mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa
Tido Mhando: Mkurugenzi wa Azam Media akikabidhi mfano wa hundi kwa katibu mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *