Klabu ya Azam FC imesema kwasasa wanaangalia michezo inayofuata hususani mchezo utakaopigwa Septemba 24 dhidi ya timu ya Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkaoani Mtwara.

Afisa Habari wa klabu, Jaffery Maganga amesema mara baada ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba kikosi cha Azam FC kimeanza mazoezi na kinatarajiwa kuondoka Alhamisi ya wiki hii kwa ajili ya kuifuata Ndanda FC.

Maganga amesema ili kujihakikishia kikosi kinafanya vizuri katika mchezo huo, kocha Zeben Hernandez ameanza kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita ili yasiweze kujirudia katika mchezo huo.

Pia Maganga amesema mpaka sasa wana majeruhi watatu ambao ni Mlinzi wa kati Serge Pascal Wawa, beki Erasto Nyoni na Aggrey Morris.

Licha ya mchezo huo wa Azam FC na Ndanda FC utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Nangwanda sijaona Mjini Mtwara, mchezo mwingine wa kiporo unatarajiwa kupigwa hapo leo ambao utawakutanisha wenyeji African Lyon dhidi ya Toto Africa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *