Klabu ya Azam Fc imeenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujiandaa na mechi ya Ngao ya jamii dhidi ya Yanga SC na ligi kuu Tanzania Bara itakayoanza mwezi Agosti mwaka huu.

Kikosi cha mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati kimefikia katika hoteli ya kitalii ya Mtoni Marine ambapo kinatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki ambazo bado hazijawekwa wazi zitakuwa na timu gani.

Azam FC: Wakishangila moja ya magoli yao kwenye mechi ya ligi kuu katika uwanja wa Chamanzi
Azam FC: Wakishangila moja ya magoli yao kwenye mechi ya ligi kuu katika uwanja wa Azam Complex, Chamanzi

Mechi ya kwanza ya Azam FC inatarajiwa kuchezwa siku ya jumatano na nyingine itachezwa siku ya jumamosi kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *