Azam FC imeendelea kung’ara kwenye mechi za majaribio za kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara, baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Kombaini ya Wilayani visiwani Zanzibar katika uwanja wa Amaan.

Mfungaji wa Azam FC alikuwa ni mshambuliaji, Fuadi Ndayisenga, aliyekuwepo kwenye majaribio, ambaye alifunga bao hilo pekee dakika ya 42.

Azam FC inatarajia kucheza mchezo mwingine wa kirafiki Jumamosi ijayo dhidi ya timu ya Jang’ombe utakaofanyika Uwanja wa Amaan visiwani humo.

Azam FC ipo visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara na mechi ya Ngao ya hisani dhidi ya Yanga SC.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *