Klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imefanikiwa kunasa saini ya winga nyota wa timu ya Medeama ya Ghana, Enock Atta Agyei, ambaye tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu hiyo.

Azam Fc imenasa saini ya mchezaji huyo baada ya kuvutiwa na kiwango chake wakati timu yake ya Medeama ilivyokuja Dar es Salaam kucheza dhidi ya Yanga SC kwenye mechi ya mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *