Klabu ya Azam inatarajia kucheza na Simba kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania Bara Januari 28 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kuelekea katika mchezo huo nahodha wa Azam FC, John Bocco amewaahidi mashabiki kupambana ili kuweza kuibuka na pointi zote tatu dhidi ya wapinzani wao hao.

Bocco amesema mchezo huo hautakuwa rahisi lakini watajituma na kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Kwa upande wake Kapombe amesema kuwa wanaendelea kujipanga vizuri na kufanya maandalizi kuelekea mchezo huo ili kupata ushindi.

Timu hizo zinakutana wakati Azam FC ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 31 ikizidiwa pointi 14 na Simba iliyojikusanyia 45 kileleni, Yanga ni ya pili ikiwa na pointi 44 huku Kagera Sugar iliyocheza mchezo mmoja zaidi ikikamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 34.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *