Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema lipo kwenye mpango wa kuwakabidhi kombe jipya la Ngao ya Jamii timu ya Azam FC  kutokana na kukabidhiwa kombe ambalo halikuwa lenyewe.

Azam walipata kombe hilo baada ya kuifunga Yanga kwa penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kumaliza 2-2 ndani ya dakika tisini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameliambia amesema waliwapa Azam ngao ambayo siyo yenyewe kutokana na kuchelewa kukamilika kwa utengenezwaji wa ngao halali ambayo walitakiwa kupewa.

Lucas amesema lile kombe ambalo waliwapa Azam siku ile walipocheza na Yanga kwenye Ngao ya Jamii halikuwa lenyewe, bali walilitoa kwa ajili ya kuziba nafasi ya kombe halisi ambalo lilichelewa kuja kutokana na kutokamilika mpaka inafika siku ile.

Pia Lucas amesema wamepanga kuwabadilishia na kuwapa kombe lao halisi ambalo walistahili kupewa ambalo hili litakuwa na thamani halisi na mwonekano tofauti kabisa na lile ambalo walilitoa awali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *