Wanamuziki wa Bongo fleva, AY, Mwana FA, Ben Pol, Linex, Msami, Barnaba na Galatone wanatarajia kutumbuiza katika onesho la Dawati Concert Agosti 13 mwaka huu.

Ben Pol
Ben Pol

Dawati Concert imeandaliwa na mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiunga jitihada za rais Dkt John Magufuli kuhakikisha kila mwanafunzi anakalia dawati.

Linex

Show hiyo inatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi Agosti 13 kuanzia saa 12 jioni na kiingilio kitakuwa shilingi 5,000.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *