Staa wa Bongo fleva, AY amewashauri watangazaji wa redio na TV hapa nchini kuchangamkia fursa kwenye vituo vya TV na redio vya kimataifa ili kuwa watetezi wa muziki wa Tanzania.

AY amesema Wanaijeria na Wasouth wamejaa kwenye vituo vya nje na ndio maana wamekuwa wakiupa kipaumbele muziki kutoka nchi zao kabla ya kuufikiria ule wa Afrika Mashariki na kwingine.

Pia AY amesema mtu wa South Africa na Nigeria atafanya rotation za mtu anayetoka kwao kwanza kabla ya kuangalia sehemu nyingine ndiyo mana wasanii wao wanakuwa juu siyo kama wanauwezo kuwashinda wasanii wa Tanzania au Kenya.

AY amesema ukiangalia katika vituo hivyo vya kimataifa hautoona Mkenya, Mganda au Mtanzania.

AY ameongeza kwa kusema kuwa ni muda sasa kwa watu wenye fani za utangazaji ni vizuri kama wakiomba kazi katika maeneo hayo ili waendelee kupata kwenye vituo hivyo vya kimataifa.

AY amedai kuwa kama Mtanzania hata yeye angekuwa anafanya kazi MTV au Trace TV ni lazima angefanya kitu kuubeba muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

AY ni mwanamuziki mongwe wa Bongo ambaye muziki wake umevuka boda la kimataifa kutokana na kufanya kazi na baadhi ya wasanii wa nje ya nchi kama vile Nigeria, Uganda, Kenya na Afrika Kusini.

Mwanamuziki ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wanaunda kundi la East Coast Team miaka ya nyuma ambapo kundi hilo lilijizolea umaaufu mkubwa kutokana na vibao vyao kubamba masikiono mwa mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *