Mwanamuziki wa Bongo fleva, AY amesema kuwa uwezekano wa kurudi kundi la East Coast Team anao King Crazy GK kama ikiwezekana kurudi.

 AY amesema uwezekano wa kundi hilo kurudi upo lakini mwenye uamuzi wa mwisho ni King Crazy GK kwasababu yeye ndiyo Amiri Jeshi mkuu wa kundi hilo.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa East Coast Team ipo hata kama yeye na FA walitoka kwenye kundi hilo na kufanya kazi zao binafsi ila kufanya kazi kama kundi itatokea lazima na itafanyika.

Kwa upande mwingine  AY amezungumzia kitendo cha GK kurudi kwenye game kwa kuamua kuimba na kusema kuwa amefanya vizuri kwenye kurudi kwake kutokana na soko la muziki kubadilika.

Kundi la East Coast Team ni kundi lililojizolea umaarufu mkubwa hapa nchini mnamo miaka ya 2000 kutokana na nyimbo zao kuwabamba mashabiki wa muziki huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *