Kesi inayowakabili viongozi wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imeendelea tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wanakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha pamoja na kughushi nyaraka ambapo kesi yao imeendelea leo mahakani hapo.

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mwambapa baada ya Wakili wa TAKUKURU, Kishenyi Mutalemwa kueleza kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Agosti 22 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika juu ya tuhuma za viongozi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *