Kesi ya madai ya utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa Simba Evance Aveva na Makamu wake,Godfrey Nyange ‘Kaburu’ imetajwa leo Julai 20 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wa Simba wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650).

Aveva peke yake aliweza kufika mahakamani hapo na kushuhudia kesi hiyo ikitajwa huku, Kaburu akishindwa kufika mahakamani kutokana na kudaiwa kuwa ni mgonjwa.

Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande baada ya kesi yao kuahirishwa na sasa watarejeshwa mahakamani hapo Julai 31, mwaka huu.

Kabla ya kesi hiyo kutajwa wanachama wa Simba walianza kufika mahakamani mapema ili kujua hatima ya viongozi wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *