Kesi ya madai ya utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa Simba Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imeahirishwa kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo imehairishwakutokana na upelelezi kutokamilika dhidi ya tuhuma za washitakiwa hao.

 Kesi hiyo iliyokuwa isikilizwe na Hakimu Victoria Nongwa imepamgwa kusikilizwa tena Agosti 7 mahakamani hapo, ambapo watuhumiwa wamerudishwa gerezani.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *