Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili viongozi wa Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imeendelea leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika upelelezi wa kesi hiyo kuwa wakweli.

Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa alisema hayo baada ya Wakili wa Serikali, Nassor Katuga kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba bado nyaraka hazijawa tayari kutoka kwa mtaalamu wa maaandishi.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa aliutaka upande wa mashtaka kuwa wakweli na kuhakikisha upelelezi unakamilika haraka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba18 mwaka huu itakaposikilizwa tena baada ya kukamilika kwa upelelezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *