Rais wa Simba, Evans Aveva ameachiwa huru baada ya kushikiliwa na Polisi tangu jana jioni kwa tuhuma za kuhamishia fedha za klabu katika akaunti yake binafsi.

Aveva amehojiwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) leo juu ya kuhamisha zaidi ya dola za Kimarekani 300,000 kutoka akaunti ya klabu kwenda akaunti yake binafsi.

Fedha ambazo Aveva anadaiwa kuhamisha ni zilizolipwa na Etoile du Sahel ya Tunisia, dola za Kimarekani 300,000 zaidi ya Sh. Milioni 600 za Tanzania kwa ajili ya usajili wa Emmanuel Okwi.

Awali, Etoile walikuwa wazito kulipa fedha hizo kwa sababu walidumu na Okwi kwa miezi sita kabla ya kushindwana na kushitakiana hadi FIFA.

okwi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *