Pambano la kina dada wawili wa familia ya Williams, Venus na Serena limemalizika kwa dada mdogo, Serena kumtandika dadaake Venus kwa seti mbili mfululizo za 6-4 na 6-4 na kushinda taji lake la saba la mashindano ya Australian Open na kuweka rekodi ya Grand Slam.

Serena mwenye miaka 35 amefanikiwa kumpita mcheza tenisi Steffi Graf aliyekuwa akishikilia rekodi ya kushinda mataji mengi makubwa tangu Grand Slams ikubali kushirikisha wachezaji wa kulipwa mwaka 1968.

Kufuatia ushindi huo Serena amerejea kileleni mwa wachezaji bora wa mchezo na kumpiku mjerumani Angelique Kerber.

Mpaka sasa ni mchezaji wa Australia, Margaret Court pekee mwenye idadi kubwa ya mataji ya Grand Slam ya mchezaji mmoja mmoja kumzidi Serena Williams.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *