Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel  amesema kuwa aamini kama Kanumba kufa na Bongo Movie imekufa ila tatizo lipo kwa wasanii wenyewe.

Aunty amesema hayo baada ya mashabiki wa tasnia ya filamu kusema kuwa toka Kanumba afariki dunia na Bongo movie nayo imekufa lakini muigizaji huyo amekanusha hayo na kusema wasanii wenyewe wamekosa ubunifu.

Pia muigizaji huyo amempongeza muigizaji mwenzake Gabo Zigamba na kusema kuwa msanii huyo ndiyo angeweza kuziba pengo la Kanumba ambaye alifariki dunia mwaka 2012.

Aunty amesema kuwa kinachosababisha Gabo asifikie nafasi ya Kanumba kwasababu soko la filamu limeshuka kwasasa kutokana na kukosa soko rasmi la kuuza filamu zao ambazo zimepungua umaarufu.

Bongo Movie kwasasa imeshuka mpaka wasanii wenyewe wamekiri hilo huku lawama wakijipa wenyewe kwa kukosa ubunifu kwenye uigizaji pamoja na ubinafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *