Staa wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amesema hayuko tayari kuolewa kwasasa na kwamba bado hajafikiria kuolewa kwa kuwa suala la ndoa linahitaji maandalizi zaidi.

Aunty Ezekieli amesema kuwa ndoa sio maigizo bali ni kitu kigumu na kinatakiwa kujiandaa vyema na kwamba siyo kwakuwa Shamsa kaolewa basi na yeye akimbilie kuolewa.

Kutokana na Aunty Ezekiel kuonekana amepotea kwenye tasnia ya filamu mara baada  ya kuwa kwenye mahusiano na Moses Iyobo ambaye amezaa naye mototo mmoja staa huyo alikanusha taarifa hizo kwa kusema hiyo siyo sababu.

Aunty alikanusha kupotea kwenye game na matukio yote ya filamu bali ameweka wazi kuwa amekua kimaisha kutoka hatua moja hadi nyingine na kwamba ndiyo maana ameamua kuachana na mambo ya ujana na kutafuta kiki.

Staa huyo amesema kwasasa ni mama na amekua ndiyo maana aonekani akifanya hayo na ndiyo maana watu wanasema amepotea kwenye game la filamu kutokanakwasasa haitaji kiki kwani wakati wake umeshakwisha.

Kwa upande mwingine Aunty amewataka wasanii wenzake ambao wanatembea utupu anawaomba waache kwa kuwa hazitawasaidia kwa kuwa hazina faida kwasasa.

Aunty Ezekiel ni staa wa Bongo movie aliyejizolea sifa kibao ndani ya nchi kutokana na kuwa muigizaji anayegusa nyoyo za mashabiki wake kutokana na uigizaji wake wa filamu za Bongo movie.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *