Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amesema kuwa anatamani kupata watoto zaidi kwa kuwa huu ndio wakati wake wa kufanya hivyo.

Aunt Ezekiel ambaye yupo kwenye uhusiano na dansa, Mose Iyobo amesema kwa kuwa ndio wakati wake wa kufanya maamuzi sahihi na haoni idadi kamili ya watoto atakaokuwa nao katika familia yake na Iyobo.

Muigizaji huyo amesema kuwa “Nilitamani kuitwa mama sasa naitwa mama, naomba Mungu anisaidie nikuze familia yangu na anibariki nipate watoto wengine kwa kuwa watoto ndiyo furaha yangu zaidi,”.

Pia amesisitiza kuwa “Mtoto wangu wa pili natamani awe wa kiume na wengine zaidi ambao hata sijui watakua wangapi watakaokuwa na jinsia yoyote nitafurahi kwa kuwa tamaa yangu ni kuwa na watoto wengi,”.

Hadi sasa hivi muigizaji huyo ana mtoto mmoja anayeitwa Cookie ambaye amezaa na dansa huyo Mose Iyobo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *