Mkali wa muziki wa Bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekuwa na “kismati’ cha kupendwa na baadhi ya mastaa nchini mpaka watu wanasema kuwa baadhi ya mastaa hao wanajipendekeza kwa Diamond.

Hivi karibuni kulikuwa na na sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Zari ambayo imefanyika visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na baadhi ya amashabiki na watu wa karibu wa Diamond pamoja na Zari akiwemo Aunty Ezekiel.

Kwenye sherehe hiyo Aunty Ezekiel aliongozana na mpenzi wake ambaye ni dansa Mose Iyobo mpaka mwisho wa sherehe hiyo.

Baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo Aunty bado alibakia Zanzibar pamoja na Kina Diamod na Zari mpaka kupelekea baadhi ya watu kusema kuwa Aunty Ezekiel anajipendekeza kwa Zari kutokana na kuwa nae muda wote.

Aunt Ezekiel akawajia juu mashabiki katika mitandao ya kijamii ambao wanadai anajipendekeza kwa Zari.

Maneno ya Aunty kwa baadhi ya mashabiki matandaoni  “Nataka niwaambie kitu kimoja maana kujibu mmoja mmoja muda huo sina ni hivi nafanya nitakalo sifanyi mtakayo, maana nina uhakika nyie mnaokaa kubishana na mimi vibanda vya mbavu za mbwa vinawashinda, so muda mnaokaa mkafatilia yangu mngeenda kutafuta yakufanya, ooh! njaa yes i say tena yes maana mnataka nibadili red kuwa yellow kwani yule si ni boss wa mkata viuno wangu au!. Sasa kama ni bosi ulitaka nibishe niseme mimi ndio bosi, basi nifungue bendi yetu acheze!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *