Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amekiri kuwa katika maisha yake amewahi kutoa mimba na hakumbuki idadi ya mimba ambazo amewahi kuzitoa, huku akifichua siri kuwa amewahi kwenda kwa waganga kwa ajili ya kazi zake za sanaa.

Aunty amesema hawezi kusema uongo kuwa hajawahi kutoa mimba, lakini kitu ambacho hakumbuki ni idadi ya mimba alizowahi kutoa.

Muigizaji huyo ambaye kwa sasa ana mtoto aliyezaa na dansa wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo amesema kwa sasa anatamani zaidi kupata mtoto wa kiume atakamuita jina la Greyson ambalo ni jina la babu yake.

Pia Aunty  ametaja idadi ya wanaume ambao amewahi kutoka nao kimapenzi huku akikanusha kutoka na marehemu Kanumba pamoja na Diamond Platnumz.

Kuhusu umri wake Aunty amesema kwa sasa ana miaka 29 anaelekea wa 30 na ni mkubwa kuliko mpenzi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *