Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amefunguka sababu ya kutoongozana na mpenzi wake Mose Iyobo kwenye uzinduzi wa filamu mpya ya Wema Sepetu ‘Heaven Sent’.

Aunty ameamua kutoa ufafanuzi huo wa kutinga peke yake katika usiku wa kuitazama filamu mpya ya shoga yake Wema Sepetu.

Muigizaji huyo amesema kuwa sababu iliyofanya Mose Iyobo kutoudhuria uzinduzi huo ni kwasababu mtoto wake Cookeis alikuwa anaumwa.

Aunty amesema kuwa  “Moses hajaja kwa sababu mtoto alikuwa hayupo sawa, so nikaona sio vizuri wote tukija huku na nikisema mimi nibaki. Wema she is my friend so inakuwa sio vizuri, nikasme awacha mie nije ye abaki,”.

Filamu ya Heaven Sent ilizinduliwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi na mastaa kibao wahudhuria uzinduzi huo akiwema Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Steve Nyerere.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *