Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund, Emerick Aubameyang kufuatia kwenda kinyume na mkataba wa kibiashara.

Aubameyang yupo hatarini kutozwa faini ya Pauni 43,000, baada ya kuvaa kinyago kilichokua na nembo ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike wakati klabu hiyo ina dhaminiwa na kampuni ya Puma.

Mshambuliaji huyo alivaa kinyago hicho wakati akishangilia baada ya kufunga bao katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Ujerumani mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Schalke 04, ambao walilazimisha sare ya bao moja kwa moja.

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma, ina jukumu la kutoa huduma ya vifaa vya michezo katika klabu hiyo na pia ni inamiliki asilimia ya hisa za uendeshaji wa klabu ya Borussia Dortmund.

Hii si mara ya kwanza kwa Aubameyang mwenye umri wa miaka 27, kuvaa kinyago pindi anaposhangilia, aliwahi kufanya hivyo kwa kuvaa vinyago vya Spiderman na  Batman siku za nyuma.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *