Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ruaruke wilayani Kibiti mkoani Pwani, Ramadhan Mzurui ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Pia watu hao wamemjeruhi kwa risasi mke wa marehemu huyo sehemu ya mguuni ambapo amekipmbiza hospitali.

Mganga wa zamu katika Hospitali ya Mchukwi Dk Emmanuel Humbi amethibitisha kkufikishwa hospitalini kwa mwanamke huyo akiwa na majeraha ya risasi kwasasa yupo katika chumba cha matibabu.

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Kibiti, Onesmo Lyanga amesema polisi wamekwenda sehemu iliyotokea tukio kwa uchunguzi zaidi.

source: Mwananchi

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *