Klabu ya Atletico Madrid imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Europa ligi baada ya kuifunga Olympique Marseille 3-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika jana.

Magoli ya Atletico yakifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 21 na 49 wakati goli la mwisho likifungwa na Gabriel Fernandez dakika ya 89.

Ubingwa huo sasa ni heshima pia kwa Fernando Torres ambaye ametangaza kuwa huu ndio msimu wake wa mwisho kuichezea Atletico Madrid.

Hilo linakuwa ni taji la pili la Europa League kwa Atletico Madrid chini ya kocha Diego Simeone ambaye pia ameiongoza timu hiyo kufika hatua ya fainali ya Champions League na kutwaa mataji ya Copa del Rey, Super Copa, Super Cup na LaLiga.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *