Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limezindua safari za ndege la shirika hilo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kuanzia leo.

Uzinduzi wa safari za ndege hizo umefanywa na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo.

Waziri mkuu amesema kuwa safari hizo zitawezesha wafanyabiashara na wananchi wengine kutoka Dodoma na kwenda katika maeneo mengine kwa urahisi.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa ATCL. Kapten Richard Shaidi ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa ujio wa ndege hizo na kwamba hiyo ni moja ya mikakati ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ya kufufua ATCL.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Bw. Emmanuel Korosso amesema hivi karibuni shirika hilo linatarajia kuanza safari za kwenda katika miji ya Tabora, Songea, Mtwara, Mpanda, Mafia na Jiji la Tanga.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa safari za Dodoma zitafanyika mara mbili kwa wiki, siku ya Ijumaa na Jumatatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *