Mkali wa miondoko ya mduara nchini, AT amefunguka kwa kusema wasanii wenzake wasiwe na uroho wa madaraka ya mzuziki kwasababu kila mtu ana nafasi yake kwenye tasnia hiyo.

 AT amesema alikaa kimya muda mrefu kwasababu alikuwa anatafakari ili atakaporudi aweze kutoa kazi nzuri zaidi na kuwabamba mashabiki wake na si kukurupuka.

Mwanamuziki huyo aliendelea kusema kuwa yeye si kama wasanii wengine ambao wanataka kusikika kila siku kwenye muziki na kutotoa fursa kwa wengine kusikika na kuwataka wasani wengine wasiwe na uchu wa muziki siyo vizuri inabidi tuwape nafasi weninge.

Pia mkali huyo amesema watu wanaosema alikuwa amepotea kwenye game hawako sahihi kwani hakuna mtu mwenye akili zake timamu na mwenye uwezo mzuri kwenye game akapotea kirahisi.

Hivi sasa AT ameachia wimbo pamoja na msanii mwenzake Peter Msechu ambao upo kwenye mahadhi ya singeli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *